Napenda kuwapongeza sana Guydon Ranch wakati nimeingia kwenye internet nikitafuta wapi ntapata Ng’ombe wa maziwa, haikuwa rahisi kwa Tanzania kupata website inayojihusisha na kuuza mifugo, nilikuwa nakutana na website za nchi nyingine tu, lakini baada ya kuendelea kutafuta kwenye internet nikakutana na Guydon Farm & Ranch website nilipo ifungua nikakutana na link ya Livestock, nilifurahi sana baada ya kufungua hiyo link nikakutana na orodha ya mifugo mnayouza na sehemu ilipo na jinsi ya Kwenda kuiona. Ahsanteni sana kwa kutuanzishia huduma hii hapa nchini Tanzania.